Mgombea kiti cha ubunge katika eneo la Jomvu kwa tikiti ya chama cha jublee Juma Renson Thoya amezitaka asasi za kiserikali kuacha kutumiwa na viongozi wa kisiasa kutatiza mikutano ya wagombea wengine.

Thoya amesema kuwa wakati wa vijana na asasi zingine za kiserikali kutumiwa kisiasa umepitwa na wakati hivyo kila mmoja apewe nafasi sawa kunadi sera zake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Jublee Nelson Dzuya amesema kuwa kama chama wameanza mikakati ya kuona wanatoa usaidizi kwa wagombeaji wao kote mashinani.

Hata hivyo Dzuya amewahakikishia wagombea wao kwamba hakutakuwa na masuala ya zoning.