Oparesheni ya nenda shule kaunti ya Kwale imewanasa zaidi ya wanafunzi 500 waliokamilisha darasa la 8 kisha kusalia nyumbani tangu wanafunzi wa kidato cha kwanza kujiunga na shule za upili.

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao wakiongozwa na Mariga Shaban wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha kuwa changizo kuu ya kushindwa kuwapeleka wanao kujiunga na shule za upili

Ni hali ambayo imewalazimu kutafuta misaada ili kukwepa sheria iliyopo dhidi ya wazazi ambao hadi sasa hawajaafikia agizo la serikali.

Ni hatua ambayo imemlazimu mbunge wa Matuga Kassim Tandaza kusimamia gharama za baadhi za wanafunzi hao kwa kima cha shilingi milioni 1.5.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kamishna wa kwale Gideon Oyagi kuamrisha machifu kuwasaka wanafunzi hao.