Mwanamme mmoja ameuawa katika club moja mjini Kilifi baada ya kuzozana kuhusu matokeo ya mpira wa soka kwenye mechi kati ya Real Madrid na Liverpool usiku wa kuamkia leo.

Walioshuhudia kisa hicho wamesema kuwa mzozo huo umeamza baada ya mashabiki wa timu hizo mbili kuanza kurushiana cheche za maneno na baada kuanza kurushiana viti na chupa.

Inaarifiwa kuwa walinzi wa club hiyo inayofahamika kama lexo walimshambulia zaidi mwanamme huyo na kupelekea kifo chake.

Maafisa wa polisi walifika mahala hapo na kuutuliza umati huo na kuuchukua mwili huo na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi.

Kwa sasa maafisa wa polisi wameshika doria katika club hiyo kwani kuna tetesi huenda wananchi wakaivamia.