Taasisi ya watoto wenye ulemavu wa kuongea, kusikia na kuona nchini imeitaka serikali kuu kuongeza bajeti ya taasisi hio ili kuhakikisha watoto walio na uwezo maalumu wanapata elimu bora.

Mwenyekiti wa taasisi hio Francis Ng’ang’a aliyekuwa akizungumza na wanahabari alipotembelea shule hio mjini Kwale, ameutaja ukosefu wa fedha za kutosha kama tatizo kuu inayosababisha vikwazo kwa watoto hao.

Akigusia swala la elimu Ng’ang’a ameelezea masikitiko yake ya kukosekana kwa chuo kikuu cha mafunzo ya walemavu wasiosikia na kuona nchini, akisema kuwa watoto wengi husalia kufanya kazi za mikono pindi wanapomaliza kidato cha nne.

Ameitaka serikali kuu kujenga chuo kikuu kwa watoto wenye uwezo huo maalumu ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu ya kutosha na kujikimu kimaisha.