Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton samboja amewataka wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa za amani ili kuepuka migawanyiko.

Kulingana na Samboja wananchi kaunti hiyo wamekuwa wakitangamana katika maisha yao bila ya kujali misingi ya ukabila au dini.

Akiongea kwenye kikao na wakaazi wa eneo la Mbololo kaunti ya Taita Taveta, Samboja amewataka wananchi kaunti hiyo kujitenga na viongozi walio na nia ya kuwagawanya na kuwataka viongozi kuuza sera zao.

Samboja ambaye anatetea kiti hicho kwa mara ya pili sasa amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa balozi wa amani wakati huu wa kampeni na hata baada ya uchaguzi mkuu, akisema maisha na udungu lazima udumu hata baada ya siasa.