Mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kutatua changamoto mbalimbali zinawakumba wakaazi wa kaunti ya Mombasa endapo atachaguliwa kuwa gavana.

Akizungumza huko Mtopanga eneo bunge la Kisauni Nassir ambaye alikuwa ameandamana na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea wa ubunge eneo hilo Rashid Juma Bedzimba, Nassir ameahidi kulinda raslimali za kaunti ya Mombasa kwa manufaa ya wakaazi.

Katika ziara hiyo Nassir pia alipata fursa ya kuelezea manifesto yake kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa ikwemo kutatua changamoto ya karo kwa wanafunzi.

Kwenye suala la Bandari Nassir amesema anaamini kuwa utendakazi wa Bandari ya Mombasa utarudishwa kwa manufaa ya wakaazi wa Mombasa na pwani kwa ujumla endapo kinara wa ODM Raila Odinga atachukua hatamu ya urais wa jamhuri ya taifa la kenya.

Nassir ametaka pesa zinazopatikana katika bandari ya Mombasa ziweze kuwanufaisha wa pwani.