Viongozi wa kisiasa na wananchi katika eneo la Bangladesh hapa Mombasa wahubiri kudumishwa kwa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa agosti tisa.

Akiungumza katika mdahalao wa viongozi kutoka vyama mbalimbali ulioandaliwa na shirika la shining hope for communities SHOFCO huko Bangladesh mkurugenzi wa shirika hilo George okeyo amesema kufikia sasa wanaendelea kuhamasisha wagombea na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini kuelewa umuhimu wa amani.



Mshirikishi wa shirika la shofco kaunty ya Mombasa Risper Achieng Ochieng amehimiza viongozi watakaochaguliwa baada ya uchaguzi mkuu ujao kuhakikisha wanatekeleza ahadi zao ikiwemo kushughulikia suala la gharama ya juu ya maisha linaloshuhudiwa kwa sasa.



Kauli ya risper imeungwa mkono na mwakilishi wa wanawake katika shirika la shofcho Rose Owino.Owino aidha amesema kuna haja ya jamii kuwezeshwa kikamilifu ili waweze kujikimu kimaisha.