Wizara ya afya hii leo inaongoza taifa katika kuadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha watoto.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni – “Kuimarisha unyonyeshaji; Elimisha na saidia”.

Kauli hiyo inahimiza kunyonyeshwa kwa watoto ili kuboresha afya na hali zao pamoja na zile za kina mama na jamii.
Unyonyeshaji watoto hutekeleza jukumu muhimu katika afya na ukuaji kwa kuhakikisha lishe bora, usalama wa chakula na kupunguza kutokuwa na usawa.

Ikishirikiana na wadau wengine, wizara ya afya itaanda hafla maalum ya kuzindua wiki hiyo ya kuwanyonyesha watoto.

Shirika la afya duniani likishirikiana na shirika la UNICEF, linapendekeza kuwa watoto waanze kunyonyeshwa saa moja baada ya kuzaliwa na kuendelea kwa miezi sita ya kwanza, bila mtoto kupewa chakula kingine.