Mgombea mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Azimio La Umoja – OKA Bi. Martha Karua amewataka maafisa watakaosimamia uchaguzi mkuu ujao kua makini na kutokubali kuhujumu zoezi hilo.

Akiongea katika kikao na wadau kutoka sekta ya elimu nchini, Karua amewataja walimu na maafisa wa usalama kama viungo muhimu wakati wa uchaguzi mkuu na kwamba sharti wahusika wote kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa ki maadili.

Karua amesema serikali ya Azimio iwapo itachaguliwa baadaye mwaka huu, itahakikisha maswala ya walimu yanaangaziwa ikiwemo mabadiliko kwenye sekta hiyo.

Amehoji kwamba serikali yao itaziba mianya yote ya ufisadi ili kuongeza fedha za kufanikisha mageuzi nchini.

Katibu mkuu wa muungano wa waalimu nchini KUPPET Akello Misori ameitaka Azimio kutekeleza mageuzi kwenye sekta ya elimu nchini na kutangaza kumuunga mkono Raila Odinga na Martha Karua ili wabuni serikali ijayo.