Huku zikisalia siku 32 kufikia uchaguzi mkuu wito wa amani unazidi kutolewa huku wakenya wakisisitizwa kuwa kudumisha amani ndio njia ya pekee ya kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza na mwanahabari wetu afisini mwake mgombea huru wa kiti cha uwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Lubna Nassir amewataka wakaazi wa Mombasa kuhakikisha kuwa wanaepuka kutumiwa kuzua vurugu na badala yake wadumishe amani.

Aidha amewasihi vijana na wakaazi wa Mombasa kwa jumla kuepuka siasa za kununuliwa kwani kupiga kura kwa kulipwa kutakiuka haki zao hali ambayo itawachangia kupigia kura viongozi ambao hawatakua waadilifu.