Baadhi ya wakaazi wa Mombasa wameandamana wakilalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa humu nchini.

Wakishiriki maandamano hayo huko Kisauni, waandamanaji hao wameitaka serikali kupunguza bei za vyakula ambavyo vinatumiwa sana na mwananchi wa kawaida.

Waandamanaji hao wamedai endapo bei za bidhaa muhimu hazitashukishwa basi hawatashiriki katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9.

Mapema wiki hii kutokana na shinikizo la wananchi wengi, waziri wa kilimo Peter Munya alisema unga wa simu utapunguzwa bei kwa shilingi mbili hatua ambayo haijachukuliwa vyema na wananchi.

Kwenye mikutano ya kampeni za wanasiasa humu nchini, ahadi za kupunguza gharama ya uchumi humu nchini zinatawala.