Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatano, alitia saini miswaada sita kuwa sheria ikiwa ni pamoja na ule wa usimamaizi wa taka.

Miswada mingine ni pamoja na mswaada wa marekebisho ya sheria ya unyunyiziaji maji mashamba, ule wa marekebisho ya sheria ya utoaji zabuni na marekebisho ya sheria ya kusimamaia vyama vya ushirika na akiba, msawaada kuhusu watoto na mswaada kuhusu usajili wa vikundi vya kijamii mwaka 2021.

Sheria mpya ya bunge kuhusu usimamizi wa taka umewekea mfumo wa kisheria wa kuhakikisha uoandoaji taka kwa njia zifaazo ili kuafikia mahitaji ya kikatiba ya mazingira safi.

Pia sheria hiyo imeweka mwongozo wa kubuni mikakati na baraza la kusimamia taka ambalo litajukumika kuongoza utaratibu wa utekelezwaji wa mpango wa kitaifa wa kusimamia taka.

Sheria ya bunge kuhusu usajili wa makundi ya kijamii kwa upande mwingine, inatoa mwongozo kuhusu usajili na usimamizi wa makundi ya kijamii.

Sheria mpya ya bunge kuhusu watoto imebainisha majukumu ya wazazi kwa watoto wao na jinsi ya kuwatunza watoto.

Sheria hiyo imeonekana kuelekeza majukumu ya ulinzi wa watoto kwa serikali na jamii kupitia kubuniwa kwa taasisi za kusimamia masuala ya watoto na waziri husika.

 Kwa hisani ya Kbc radio taifa