Mgombea wa kiti cha ugavana wa Kwale kupitia chama cha ODM Prof. Hamadi Boga ameitaka serikali ya kitaifa kufungua anga ya ndege za kimataifa ili kuimarisha sekta ya utalii katika eneo la Pwani.

Boga amesisitiza haja ya serikali kuu kuziruhusu ndege za kimataifa kutua katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa ili kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka Pwani.

Wakati huo huo, mwanasiasa huyo ameishinikiza serikali hiyo kuwekeza katika ujenzi wa hoteli za kimataifa ili kuwavutia watalii humu nchini.

Kwa upande wake mgombea wa kiti hicho kwa tikiti ya chama cha Wiper Balozi Ali Mwakwere ameahidi kulishughulikia tatizo la unyakuzi wa ardhi uliokithiri kaunti ya Kwale.

Wawili hao wameyasema hayo katika mdahalo wa wagombea wa ugavana wa Kwale ulioandaliwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA