Mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa anazidi kutoa wito kwa serikali ya kaunti kuondoa ada zinazotozwa ardhi za sehemu za ibada.

Akizungumza katika kanisa la Shalom hapa Mombasa Nassir amesikitishwa kusikia malalamishi kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa kanisa kuibua madai kuwa serikali ya kaunti Mombasa kupitia wizara husika inatoza ada za ardhi katika sehemu za ibada.

Hata hivyo ambaye anaazimia kurithi kiti cha ugavana kutoka kwa gavava Ali Hassan Joho ametoa uhakikisho na kuahidi kuwa katika serikali ya kaunti atakayoiunda endapo atachaguliwa kuwa gavana atafuatilia kuhakikisha kuwa hakuna ardhi katika sehemu za ibada itakayotozwa ada yoyote na serikali ya kaunti.

Haya yanajiri huku zikiwa zimesalia siku 22 kufikia uchaguzi mkuu.