Huku kampeni za siasa zikionekana kupamba moto mwaniaji wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ametoa wito wa Amani msimu wa uchaguzi.

Akizungumza na wakaazi hapa Mombasa wakati wa hafla ya mchezo wa kandanda katika uwanja wa Ronald Ngala Nassir amesema kuwa sasa ni wakati kwa wananchi kujieka mbalimbali na viongozi wanaoendeleza siasa za chuki badala yake wahubiri Amani.

Nassir ambaye anaamini kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania ugavana kaunti ya Mombasa,amesema yuko tayari kuwaalika wapinzani wake siku ya kuapishwa kwake.

Nassir atamenyana na Hassan Omar Sarai wa UDA,Hezron Awiti wa VDP,William Kingi wa PAA,Daniel Munga Kitsao Mgombea huru,Said Abdallah wa Usawa Kwa Wote,Shafi Makazi wa UPIA na Antony Chitavi wa chama cha UDP