Viongozi wa chama cha ODM hapa Mombasa wanashikilia msimamo wao wa kupigia debe mfumo wa 6 piece katika uchaguzi mkuu ujao.

Wakizungumza na wakaazi wa eneo bunge la Likoni wakati wakiendeleza kampeni za kumpigia debe mgombea wa urais chini ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ,viongozi hao wakiongozwa na mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema hawezi kubali kuregeshwa nyuma na viongozi wenye kutumia ubabe ili kuingia katika uongozi na kuchafua chama cha ODM.

Kulingana na Nassir, Mombasa itasalia kuwa ngome ya ODM akisema hawatakubali kamwe watu wachache wavuruge mji wa Mombasa.

Kwa upande wake mbunge wa Likoni Mishi Mboko na mgombeaji wa uwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa ZamZam Mohammed wamewarai wakaazi wa Mombasa kuepuka kuhadaiwa badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kuhakikisha kuwa wanawachagua viongozi wa ODM na Raila Odinga kama rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya.