Mwaniaji wa ubunge eneo la Nyali kwa tiketi ya chama cha ODM chini ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Said Abdalla amemkemea vikali aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko kwa kile anachokisema ni kuvuruga siasa za Mombasa.

Akizungumza na wakaazi wa eneo bunge la Nyali wakati akiendeleza kampeni za kupigia debe muungano wa Azimio, Said hata hivyo amesema ujio wa Sonko hauwezi kuwa tishio kwa muungano wa Azimio.

Sonko ambaye aligura muungano wa Azimio na kujiunga na muungano wa Kenya Kwanza baada ya kuzuiliwa na mahakama kuwania kiti cha ugavana Mombasa.