Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amewahakikishia wakaazi wa eneo bunge hilo kwamba kwa ushirikiano na gavana mteule Abdul Swamad Nassir kwamba watahakikisha kushugulikia tatizo la ardhi kikamilifu katika maeneo mbali mbali ya Jomvu.

Badi amesema kuwa wakaazi wa Jomvu walifanya maamuzi ya busara kumchagua kwa mara ya tatu wakijua kuwa atawafanyia kazi bila ubaguzi.

Ameongeza kusema kuwa pindi tu watakapo anza kazi watashugulikia masuala ya hati miliki za ardhi ambacho kimekua kitandawili cha siku nenda siku rudi katika eneo hilo.