Maandalizi ya sherehe ya kuapishwa kwa gavana mteule kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir na naibu wake Francis Thoya yanaendelea katika bustani ya MamaNgina hapa Mombasa.

Vikosi vya maafisa wa kaunti ya Mombasa,na vikundi mbali mbali vya kwaya vinaendelea kufanya mazoezi ya kuwakilisha na kuwatumbuiza wageni mashuhuri katika hafla hiyo ambayo imepangwa kufanyika siku ya Alhamisi wiki hii.

Viongozi mbali mbali wanaounga mkono muungano wa Azimio la Umoja One Kenya na viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza wote wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Hata hivyo haijabainika kuwa iwapo rais mteule William Ruto atahudhuria sherehe hiyo siku ambayo atakuwa katika ziara yake hapa jijini Mombasa katika bandari ya Mombasa KPA.