Polisi wamelazimika kuwarushia vitoa machozi wafuasi wa Azimio.

Wafuasi hao walikuwa wakiandamana na wabunge wa muungano huo hadi makao makuu ya IEBC kulalamikia shirika la uchaguzi kuhusu kusimamishwa kazi kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Ruth Kulundu.

Wiki iliyopita, IEBC ilimsimamisha kazi Kulundu kwa madai ya kuhasi tume hiyo.

Haya yanajiri siku chache baada ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga na vinara wa upinzani kuapa kupiga kile walichokiita mpango wa kuwahujumu baadhi ya wafanyikazi wa IEBC.

Hii ni baada ya chama cha Farmers Part kuwasilisha ombi Bungeni la kuwatimua makamishna Justus Abonyo, Irene Cherop na Francis Wanderi.

Kulundu alishutumiwa na IEBC kwa kutotii na kusaidia shughuli za makamishna wanne waliopinga tangazo la matokeo ya urais na kuyataja kuwa yasio wazi.