Serikali ya kaunti ya Mombasa inapanga kuanzisha mchakato wa kuwa na uchumi wa masaa 24 kuanzia Jumatatu Jumalijalo.

Akizungumza kwenye kikao na wa wakilishi wadi afisini mwake gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema tayari serikali yake imeanza mchakato wa kuweka Taa mjini na taa katika Soko zilizopo ndani ya kaunti ya Mombasa ili wafanyibiashara waweze kufanya shughuli zao za kikazi masaa 24.

Nassir amesema atashirikiana na wakilishi wadi pamoja na Wadi Admistrators ili kuona kuwa hatua hiyo ya kuwa uchumi wa masaa 24 inafaulu.