Mume wa gavana wa Meru Kawira Mwangaz sasa anadai amekuwa akifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia.

Murega Baichu ambaye alizungumza katika Mahakama ya Milimani siku ya Ijumaa alisema kuwa amepigwa marufuku kupata lifti kutoka kwa gari rasmi la mkewe na kumlazimisha kutumia bodaboda.

Pia anadai kuwa hawezi kulala katika makazi yao rasmi kwa sababu yeye si afisa wa serikali.

Sasa anataka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imwambie mipaka yake kwa mkewe ni nini.