Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad shariff Nassir amejiunga na waumini wa dini ya kikiristo wa Kanisa la Seventh day adventist hapa Mombasa katika maandamano ya kutoa hamasa kwa jamii dhidhi ya dhuluma za jinisia, Rangi na Ukabila yaliyo andaliwa na Kanisa hilo.

  
Akiwahutubua wakaazi kabla zoezi hilo kuanza , Nassir aliwapa kongole Washirika pamoja na wakaazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuihamasisha jamii dhidi ya kukabiliana na dhulma hizo. 
 
Nassir ameiomba jamii kushirikiana Viongozi walioko serikali pamoja na viongozi wa kidini ili kuona kuwa visa vya dhulma za jinsia hapa Mombasa na Kenya kwa ujumla vinakomeshwa.