Kufuatia uteuzi uliofanywa na gavana wa Kwale Fatuma Achani wa nafasi za ktibu wa kaunti, mawaziri na mwanasheria wa kaunti, sasa bunge la kaunti ya Kwale limetoa tarehe rasmi za kuwapiga msasa maafisa hao.


Kamati ya masuala ya uajiri ya bunge la kaunti hio imeratibu mnamo tarehe 3 mwezi ujao wa Novemba kuwapiga msasa Ali Abdalla Mondo (waziri wa Utalii), Saumu Mahaja (waziri wa Mazingira), Roman Mwangome (waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi), na Tamasha Nyawa (waziri wa Huduma za Umma na Utawala).

Mnamo tarehe 4 mwezi huo watakaofika mbele ya kamati hito ni Francis Mwastahu Gwama (waziri wa Afya), Mishi Mwakaole (waziri wa Elimu), Ali Joto Mwachirumi (waziri wa barabara), pamoja na Hemed Ramadhan Mwabudzo (waziri wa Maji).

Kamati hiyo itahitimisha shughuli zake mnamo tarehe 5 kwa kupiga msasa Bakari Hassan Sebe (Waziri wa Fedha), Sylvia Chidodo (katibu wa kaunti), Salim Gombeni (mwanasheria wa kaunti) na kisha Francisca Kilonzo (waziri wa Huduma za jamii na ukuzaji talanta).

Maafisa hao 10 wanatarajiwa kuanza rasmi majukumu yao ya kikazi baada ya kuapishwa, iwapo wataidhinishwa na Kamati ya masuala ya uajiri ya bunge la kaunti ya Kwale.