Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir anapanga kufanya ukaguzi kubaini wafanyikazi hewa waliokuwepo tangu serikali ya kaunti iliyopita.

Akizungumza afisini mwake Nassir amesema tayari ameiandikia barua tume ya huduma za umma kuishurutisha kufanya ukaguzi kuhusiana Suala la wafanyikazi hewa.

 

Kauli ya Nassir inajiri baada ya kuinea kwa ripoti kuwa takribani shilingi bilioni 3 zilitumika kulipa wafanyikazi hewa katika serikali ya kaunti iliyopita.

Hata hivyo Nassir ameeleza kuwa katika harakati za kutaka kubaini ukweli wa ripoti hiyo na mwenye kuandika,aliarifiwa kuwa ilikuwa ni ripoti ya tangu mwaka wa 2013 serikali mpya ya kaunti ilipofanya ukaguzi wake baada ya kuchukua uongozi kutoka kwa serikali iliyokuwepo ya Manispaa Wala si ripoti ya hivi karibuni.