Gavana wa Kaunti ya Mombasa, Abdulswamad Shariff Nassir aweka wazi akisema atatangaza nafasi za mawaziri hivi karibuni bila ya upendeleo.

 Akizungumza afisini mwake hii leo,Nassir amesema kuwa ataweka wazi na kutangaza nafasi hizo kwa yeyote mwenye kutaka kutuma maomba.

 Nassir amesema kuwa anaamini kuwa kila mtu ana haki ya kupata ajira,akisema nafasi hizo zitatangazwa bila ya ubaguzi.

 Katika suala la kucheleweshwa kwa mishahara Nassir amesema tayari ameshirikiana na mashirika ya kifedha ikiwemo Baadhi ya Banki nchini ili kuhakikisha kuwa tatizo la kuchelewesha kwa mishahara ya wafanyikazi wa kaunti linazikwa katika Kaburi la Sahau.