Idara ya afya eneo bunge la Rabai, imehimiza ushirikiano na wakaazi kukabili ugonjwa wa saratani unaoendelea kuathiri wengi eneo hilo.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa afya wa Rabai, daktari Richmond Mudindi, hulka ya wakaazi kukosa kufanya uchunguzi mara kwa mara umepelekea wengi kupoteza maisha.

Mudindi amehimiza wakaazi kujitokeza kupata kupata huduma za afya bila malipo siku ya Jumamosi ikiwa ni njia ya idara hiyo kwa ushirikiano na wadau wengine kukabiliana na magonjwa ya saratani.

Wakati huo huo, afisa huyo wa afya amedokeza kuwa kwa udhamini wa shirika la naledy, wananuia kuandaa matibabu kwa wakaazi wa Rabai katika shule ya upili ya Rabai.

Aidha, Mudindi amesisitiza haja ya wakaazi kujitokeza kufanyiwa uchunguzi na kupata ushauri nasaha kuhusu kukabiliana na ugonjwa wa saratani katika jamii.