Watu watatu wamepoteza maisha katika ajali eneo la kwa Kazuri mjini Kilifi kwenye barabara ya Kilifi Malindi.

Akithibitisha ajali hio, kamanda wa polisi katika eneo la Kilifi Kaskazini Keneth Maina amesema kuwa ajali hiyo imehusisha Tuktuk na lori baada ya kugongana ana kwa ana.

Maina ameongeza kuwa watu wengine ambao wamenusurika kwenye ajali hiyo wanaendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya rufaa ya Kilifi.

Kamanda huyo amewataka madereva kuwa makini wakati wanapokuwa barabarani.