Kufuatia kukithiri kwa vurugu kila wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu, sasa vijana wametakiwa kutokubali kutumiwa na wanasiasa.

Kauli hii imetolewa na mshirikishi wa shirika la kijamii la Samba sports Youth agenda Mohammed Mwachausa.

Ameweka wazi kuwa mara nyingi vijana hutumika na wanasiasa kwa sababu ya ukosefu wa ajira.

Mwachausa ametaja ukosefu wa ajira na umaskini kuwa chanzo cha vijana kutumiwa na wanasiasa katika kutekeleza vurugu.

Amehimizwa kuunda vikundi vya miradi ya maendeleo ili kufaidi fedha kutoka kwa serikali na mashirka mbalimbali ili kuboresha maisha ya vijana na jamii kwa jumla.

Vilevile Mwachausa amesema kuwa miradi kwa vijana itasaidia pakubwa kupunguza visa vya uhalifu, utumizi wa mihadarati na kukomesha ghasia ambazo mara nyingi huhusishwa vijana.

Kufikia sasa zaidi ya vijana 200 wa maskani wamepokea mafunzo ya ujuzi wa kujitegemea kimaisha kupitia biashara.

Kwa upande wa baadhi ya vijana waliofaidika wameweka wazi kuwa miradi wanayoendeleza katika vikundi imewanufaisha badala ya kukaa ovyo maskani.

Wakiongozwa na Ismael Mazuri vijana hao wamedokeza kwamba mradi huo umeweza kuwanasua kutokana na utumizi wa dawa za kulevya.