Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Likoni wameanzisha uchunguzi kuwasaka majambazi wanaodaiwa kukivamia na kuiba katika kituo kimoja cha mafuta.

Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi wa eneo hilo Joseph Karanja amesema majambazi hao wanaodaiwa kuwa wanne waliwavamia na kuwafunga kwa kamba wafanyakazi wa kituo hicho mwendo wa saa kumi usiku.

Majambazi hao wanadaiwa kukivunja chumba kilichokuwa na pesa na kubeba kiasi kisichojulikana cha pesa na kukimbilia vichochoroni.

Wakati uo Karanja amethibitisha kwamba hakuna mfanyakazi aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo na kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.