Wakaazi wa Garsen kaunti ya Tana Riveriver wameonywa dhidi ya kujihusisha na siasa za mgawanyiko kwa msingi wa dini na kabila.

Siasa hizo zimetajwa kujenga chuki na migawanyiko miongoni mwa wanajamii katika kaunti hiyo.

Akiongea kwenye ufunguzi wa msikiti mjini Minijila, Imamu wa msikiti wa Oda, sheikh Ahmed Dido, amesema Siasa za ukabila zinazoendeshwa huko Tana Delta zimewapelekea waumini wa dini ya kiislamu kutengana hata kwa mambo ya dini licha ya kuwa wanaabudu kabila tofauti katika ya msikiti mmoja.

Amewasihi wanasiasa kuwacha kuwatumia vijana kuzua vurugu wakati huu wanapoelekea kwa siasa ni makosa.

Amewataja wanasiasa wanaotumia vibaya vijana akisema niwale ambao hawana moyo upendo na maendeleo kwa jamii.

Kwa upande wake katibu msimamizi katika wizara ya usalama wa ndani Balozi Hussein Dado amesema wizara hiyo imeweka mikakati mwafaka ya kiusalama husasan wakati huu taifa linapokaribia uchaguzi mkuu ujao.