Mkurugenzi wa Shirika la maswala ya kijamii la Sports Connect Foundation Athunus Mdoe Tangai amewaomba wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao wakati huu ambapo wanafunzi wako kwenye likizo.

Akizungumza na mwanahabari katika kaunti ya Mombasa Mdoe amesema kuwa ni wakati mwafaka wa wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwazuia kujiingiza katika mambo maovu ikiwemo uraibu wa dawa za kulevya kwa vijana wa kiume.

Amewataka watoto wakike kupewa ushauri bora pamoja na kupewa mahitaji yao ya msingi akitaja kuwa hali hiyo itawaepushia na kupata mimba za mapema kwa wasichana ikizingatiwa kuwa likizo hiyo imeambatana na shamrashamra za sherehe tofauti tofauti.

Aidha amewataka wanafunzi kuwa watulivu wakati huu wa likizo na kufuata maelekezo kutoka kwa wazazi na walezi wao.

Wakati uo huo amesema kama shirika kuna mikakati mbalimbali ambayo wameweka kuhakikisha kuwa watoto hawatakuwa na wakati wa kuzurura mitaani ikiwemo mashindano ya kandanda na kuonesha talanta zao tofauti