Huku wakenya wakiendelea kusherehekea likizo ya mwezi wa Disemba,wasafiri wengi wametatizika kutoka jijini Nairobi hadi Mombasa.

Usafiri kwa njia ya reli ya kisasa SGR imejaa huku magari pia yakishuhudia hali hiyo hiyo.

Ni kutokana na hali hiyo ambapo shirika la ndege la Skyward Express limetoa nafasi zaidi za usafiri kutoka kituo cha ndege cha Wilson hadi Mombasa,Ukunda,Malindi na Eldoret kwa shilingi 4,950.

Huku safari kutoka Wilson hadi Lamu na Lodwar ikiwa shilingi 6,950. Ambapo wasafiri wanaweza kukata nauli zao kupitia tovuti ya shirika hilo.

Toleo hilo ni la hapo kesho tarehe moja mwezi January mwaka wa 2022.