Wakaaazi wa Garsen kaskazini kaunti ndogo ya Tana Delta kaunti ya Tana River wameshauriwa kujitahadhari na kuwatahadharisha watoto wao dhidi ya kuoga na kucheza ndani ya maji wakati huu kuna mafuriko.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama huko Galma, Mgawa Buya, amesema kwa sasa maji yamejaa huko sehemu za Maziwa, Kiembe, Sera na Abaganda na kwamba yako na wanyama hatari.

kutokana na hali hiyo, Buya amewaomba wazazi kuwachunga na kuwafuatilia watoto wao mahali wanakoenda wakati huu wako majumbani kwa likizo ya Disemba ili kuepuka majanga yatokanayo na mafuriko.

Wakati ou huo Buya, amewasihi wale wanaoendeleza shughuli zao ndani ya maji kuwa waangalifu zaidi kwa kujilinda kutokana na hatari ya wanyama wa majini.