Wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta wameombwa kujisajili katika makundi ya kijamii ya kulinda misitu ili kuendeleza juhudi za serikali za kuhifadhi na kutunza misitu.

Akizungumza na wanahabari afisa wa idara ya misitu kaunti ndogo ya Voi Kadenge Mwatete amesema kuwa makundi ya kijamii yanayoishi karibu na misitu yanafaida pakubwa sana katika kulinda misitu nchini.

Aidha ameongeza kuwa jamii inayojihusisha na utunzaji wa misitu hufaidika na kujiimarisha kiuchumi kutokana na shughuli mbali mbali kama ufugaji wa nyuki na upanzi wa nyasi.

Hata hivyo Kadenge amesema kuwa changamoto kubwa sana inayoathiri misitu katika kaunti hio ni uchomaji wa makaa na watu kuwasha moto misituni kufuatia imani potofu.

Mwandishi:Rose Bela Tawa