Mbunge wa Mvita Abdul Swamad Sharif Nassir anapania kuzindua mradi wa lishe kwa watahiniwa katika shule za upili na zile za msingi ndani ya kaunti ya Mombasa pindi tu mitihani yao wa mwisho itakapoanza.

Kulingana na Nassir mradi huo utasaidia pakubwa watahiniwa wengi kwa kile anachosema kuwa mara nyingi watahiniwa hupoteza muda mwingi kwenda nyumbani kusaka chakula hususani wale wanaoishi maeneo ya mbali na hata kuunda mazingira bora kwa watahiniwa.

Watahiniwa hao wanapojiandaa kwa mitihani hio ya kitaifa, baadhi ya viongozi hapa Mombasa wameanzisha mchakato wa kusambaza kadi za heri njema katika mitihani.

Zoezi hilo ambalo linalofanywa kwa hisani ya mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir linalenga kuwafikia watahiniwa wote katika shule za msingi ndani ya kaunti ya Mombasa kama njia moja wapo ya kuwapa motisha wa kufanya vyema.