Wananchi katika eneo la Ruruma eneo bunge la Rabai wamepata vyeti vya kumiliki ardhi katika harakati za kukabiliana na masaibu ya ardhi.

Kwenye hafla ya kupeana vyeti hivyo takribani elfu mbili mia moja,gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wakazi wote wanapata vyeti hivyo.

Kingi amebaini kuwa upimaji zaidi wa ardhi unaendelea katika eneo bunge hilo.

Gavana huyo amebaini kuwa swala la ardhi ni miongoni mwa agenda zake ambazo alitaka kuzitimiza hasa katika kipindi chake cha uongozi.

Naye mgombea kiti cha ubunge katika eneo hilo Kenga Mpe amesema kuwa atashirikiana na serikali ya kaunti kutoa vyeti zaidi vya kumiliki ardhi pindi tu atakapochaguliwa kama mbunge wa eneo hilo.