Joto la kisiasa linaendelea kushuhudiwa hapa pwani huku gavana wa kaunti ya Kilifi Amason kingi akiendelea kuuza sera za chama cha PAA yaani pamoja African alliance.

 Kingi ameendeleza mchakato huo katika eneo la Rabai kisurutini huku akiwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa masaibu ya wapwani hasa tatizo la ardhi litapata suluhu.

 Amesema kuwa kujiunga kwa chama hicho katika azimio ni dhihirisho tosha kuwa wapwani watakuwa kwenye serikali.

 Wakati huohuo gavana huyo ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho amewarai wakazi wa Rabai kumpigia kura za urais Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu ujao.