Wakaazi katika kanda ya Pwani na taifa zima wamehimizwa kumpatia mwanamke nafasi za uongozi ili aoneshe uwezo wake wa kuihudumia na kubadilisha maisha ya jamii mashinani.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa Shirika la kupambana na uraibu wa mihadarati la REACHOUT CENTRE TRUST Taib Abdulrahman amesema kuwa ipo haja ya wanawake katika jamii kupewa  nafasi ili waeza kuonesha uwezo wao wakuhudumia jamii.

Ameyasema haya kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake ulimenguni katika ofisi za shirika hilo ambapo kumekuwa na ufunguzi wa ofisi mpya.

Katika mikakati ya kupambana na utumizi wa mihadarati miongoni mwa wanawake, Taib amesema kwamba shirika hilo limeweka mikakati mwafaka ya kuimarisha maisha ya wanawake waliyoathirika na uraibu wa mihadarati kanda ya Pwani ili kuona kuwa wanakuwa watu bora.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya nchini NACADA  Victor Okioma amepongeza juhudi zinazoendelezwa na shirika hilo la REACHOUT katika kupambana na matumizi ya mihadarati.

Aidha Okioma amewataka wazazi kanda ya Pwani na taifa zima kuwajibikia majukumu yao katika malezi ya wana wao ipasavyo na kwamba ndio njia mwafaka ya kuwaepusha na utumizi wa mihadarati.

 Mwandishi:Ibrahim Mudibo