Mgomo wa wahudumu wa afya kaunti ya Mombasa umeingia siku ya tatu hii leo.

Wakizungumza na wanahabari, wakiongozwa na katibu mkuu wa maafisa wa mahabara kaunti ya Mombasa daktari Moses Maingi, amesema kuwa hadi sasa serikali ya kaunti imedinda kutekeleza matakwa yao kikamilifu na kwamba mgomo huo utaendelea.

Wakati uo huo, Maingi ameitaka serikali ya kaunti kutowatishia wahudumu hao kwa kuandaa mgomo akisema kuwa ni haki yao na kwamba wamefuata hatua za kisheria.

Kauli yake imeungwa mkono na naibu muweka hazina wa KMPDU kanda ya Pwani daktari Mariam Mwajumla akiwataka wakaazi kutowalaumu kwa kusitisha huduma katika hospitali za umma.

Mariam amesema kwa sasa wahudumu wanaoendelea na kazi ni wale walioajiriwa na serikali ya kaunti kwa kandarasi katika vitengo vya huduma za dharura pekee.

 Mwandishi:Ibrahim Juma Mudibo