Maafisa 9 wa KDF wameuwawa baada ya gari walimokuwa wakisafiria kulipuliwa baada ya kukanyaga kilipuzi huko Gedo Somalia.

Kulingana na wakuu wa kitengo hicho cha KDF ni kwamba maafisa wengine 5 wamejeruhiwa kwenye mkasa huo uliotokea hapo jana mchana.

Kilipuzi hicho kinaaminika kuwekwa kandokando ya barabara na kundi la Alshabaab katika eneo hilo.

Lori hilo lililolipuliwa lilikuwa limetoka katika eneo la kuchota maji humu nchini Kenya na lilikuwa likipeleka maji hayo kwa matumizi huko Somalia kabla ya tukio hilo kufanyika mwendo wa saa saba za mchana.

Maafisa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini jijini Nairobi kwa matibabu zaidi.