Naibu rais Dr.William Ruto amekashifu vikali hatua ya serikali ya kuchukua pesa iliyotengewa kununua mbolea wakulima na kuzifanyia kazi nyengine.

Akiwahutubia viongozi mjini Kilifi Ruto amesema kuwa hali hiyo itafanya kuzorota kwa sekta ya kilimo nchini.

Ameongeza kuwa ataimarisha sekta ya kilimo na kuzalisha chakula kwa wingi pindi tu atakapochukua uongozi wa nchi hii.

Ameahidi pia kuimarisha biashara ndogondogo kwa kuwapa mtaji ili kukabiliana na umaskini.