Imebainika kuwa tatizo la ardhi kaunti ya Mombasa kuwa miongoni mwa changamoto kuu zinazowakumba wakaazi wa kaunti hii.

Haya ni kwa mjibu wa mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir.Kauli ya Nassir inajiri baada ya wakaazi wa maeneo ya kibarani kulalamikia suala kusumbuliwa na bwenyenye anayedai kutaka kunyakua ardhi eneo hilo.

Aidha Nassir amewaonya vikali baadhi ya mabwenyenye walio na nia ya kunyakua mashamba ya wakaazi wa kaunti ya Mombasa.