Wakaazi wa eneo la Mwakirunge eneo bunge la Kisauni wamelalamikia ugumu wa wao kupata huduma ya afya eneo hilo.

Wakizungumza huko Marimani Wadi ya Mwakirunge, wakaazi hao wakiongozwa na Matano Siwatu wameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa hospitali eneo hilo uhaba wa dawa pamoja na uchache wa wahudumu wa afya umelemaza pakubwa utekelezaji wa huduma bora ya afya kwa wakaazi.

Pia wamelalamikia tatizo la Jaa la Takataka katika eneo hilo na kusema watoto wengi wamekuwa wakichakura takataka badala ya kwenda shule.

Wametoa wito wa kuwekwa ua ama ukuta uzunguke jaa hilo ili kuwazuia watoto kufika kuingia jaani humo sawia na kuepuka kuibuka kwa mkurupuko wa maradhi mbali mbali.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kulitatua tatizo hilo ili wakaazi waishi katika mazingira salama.

Wakati huo huo ameeleza mikakati ya kujengwa kwa kiwanda cha umeme eneo hilo ili wakaazi wanufaike.