Walimu na wazazi eneo bunge la Mvita wamepongeza juhudi za mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kwa mradi wa vitabu vya marudio, shajara pamoja na Lishe kwa watahiniwa.

Akizungumza na mwanahabari wetu naibu mwalimu mkuu wa shule ya Memon Academy hapa Mombasa Hassan Ahmed Ali ameeleza furaha kufikisha jumla ya alama 350 kwa watahiniwa 84 waliokalia mtihani huo huku takribani watahiniwa 11 wakipata juu ya alama 400.

Mtahiniwa wa kwanza katika shule hio alipata alama ya 416.

Wanafunzi 2 pekee wamepata alama chini ya 250.

Kulingana na Ahmed mradi wa vitabu vya marudio, shajara za shule na lishe kwa watahiniwa kupitia kwa Nassir ulichangia pakubwa kuimarika kwa matokeo hayo.

Ruweida Kasim, mtahiniwa bora shuleni humo aliyepata alama 416 anaeleza jinsi alivyosaidika kuboresha matokeo yake.

Mariam Kassim Ahmed ni mamake Ruweida na amesema kwamba ni sharti kwa wazazi, wanafunzi pamoja na walimu washirikiane kwa ajili ya matokeo bora.

Shule ya msingi ya Ganjoni, St.Agustin,Memon ni miongoni mwa shule hapa Mombasa zilizotoa matokeo bora.

 Mwandishi:Ibrahim Mudibo/Mkala Seifu