Shule binafsi ya msingi ya Teman Junior iliyoko eneo ya Bamburi hapa Mombasa imeng’aa katika mtihani wa kitaifa kwenye matokeo ya KCPE.

Rebecca Mkoli amejizolea alama 419 na Shamsa Hassan amepata alama 412.

Wanafunzi wengine waliopata alama 400 na ushei katika shule hiyo ni pamoja na Emon Oyoo, Fatuma Adan na Venus Wendo.

Mkurugenzi wa shule hiyo Mercy Mwakwenda ameonyesha furaha yake na kutaja matokeo hayo kuwa yameletwa na ushikiano baina ya wakurugenzi, walimu, wazazi na wanafunzi.

Kadhalika, amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa ushirikiano na zaidi kumhusisha Mungu katika kuimarisha matokeo.

Licha ya matokeo hayo mazuri katika shule hiyo, Bi Mercy amesema matokeo ya mwaka huu vilevile yameathiriwa na tandavu ya korona.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu Gaystone Mwang’ombe amesema kuwa nidhamu na bidii kwa wanafunzi, kukamilishwa kwa mtaala kwa wakati kumechangia ubora matokeo hayo.

ShyMwang’ombe amesema kuwa walimu walifunga nira kukamilisha mtaala ikizingatiwa kuwa kipindi kirefu kilimezwa na janga la korona.