Mzozo mkali unaendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Kilifi kuhusiana na kura za mchujo wa chama cha Odm unaotarajiwa kufanyika jumanne juma lijalo.

Mzozo huo umechipuka katika wawaniaji wa uongozi wa ugavana baada ya Gedion Mungaro kutaka kupewa tiketi ya moja kwa moja.

Mungaro anapambana na spika wa bunge la Kilifi Jimmy Kahindi.

Kulingana na wakereketwa wa chama hicho,Mungaro anawasiwasi kuwa huenda akaangushwa kwenye mchujo huo kwani Jimmy aliandikisha wanachama wengi mashinani.

Naye mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire amesema kuwa uchaguzi huo wa mchujo utakuwa wa wazi na haki.