Wagonjwa wanaotafuta huduma za ugonjwa wa sehemu nyeti za kiume na kike yaani Urology kaunti ya Taita Taveta sasa wamepata afueni baada ya wizara ya afya ya kaunti hiyo kuweka huduma hizo katika hospitali ya Rufaa ya Moi.

Kulingana na waziri wa afya kaunti ya Taita Taveta John Mwakima ni kuwa wagonjwa wengi ambao wako na tatizo la kufunga mikojo wamekuwa wakisafiri na kupoteza fedha nyingi kutafuta huduma hiyo ila kwa sasa huduma hiyo inapatikana.

Waziri huyo ameongeza kuwa wizara hiyo itaendelea kuhakikisha inatoa huduma za afya Karibu na mwananchi huku akiwataka wananchi kaunti hiyo kukumbatia miradi ya afya.

Huku akipuuzilia mbali kuwa ugonjwa huo huwashika wazee pekee.