Huenda tatizo la ardhi linalo wakumba wakaazi wa Kwa Bullo eneo bunge la Nyali likafikia kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Hii ni baada ya mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji katika bunge la kitaifa aliyepia mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kuingilia kati na kuahidi kulipeleka suala hilo bungeni wiki hii kujadiliwa.

Wakaazi wa eneo hilo aidha ni kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi kwa hofu ya kufurushwa kutoka kwenye makaazi yao licha ya wao kuishi katika shamba hilo kwa Zaidi ya miaka 10 sasa.

Nassir amesikitishwa kuona kuwa wakaazi wa shamba hilo la Kwa Bullo wanaamrishwa kulipa shilingi milioni ili kuishi kwenye makazi yao kinyume na ada inayohitajika baina ya shilingi laki 3 na 5.

Kadhalka Nassir ametaka kuwetengwa kwa mgao fedha utakao simamia matatizo ya ardhi.

Hata hivyo Nassir amewakashifu baadhi ya viongozi wa kisiasa waliomuita seneta wa Kaunti ya Siasa James Orengo kama mnyakuzi wa ardhi.

Kulingana na Nassir,Orengo amekuwa mstari wa mbele kutetea wakaazi kutoka maeneo mbali mbali kuhusiana na suala la ardhi ikiwemo wakaazi wa shamba hilo la Kwa Bullo linalozozaniwa.

Haya yanajiri huku Nassir akimtaja gavana Joho kama mjumbe wa kwanza kuliwasilisha suala hilo bungeni hapo awali alipokuwa mbunge wa Kisauni.