Ali Hassan Mwakulonda ndiye atakaepeperusha bendera ya Odm kwenye nafasi ya ubunge wa Msambweni uchaguzi ujao baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mchujo wa chama hicho kwa kujizolea kura 1155 huku akifuatwa na Shee Mahmud kwa kura 967, wa tatu akiwa Sharlet Akinyi akiwa na kura 653.

Akizungumza baada ya kutangaza matokeo hayo msmamizi wa uchaguzi huo wa odm Solomon Wachira Njeru amewashukuru walioshiriki uchaguzi huo akisema kwamba wameshirikiana vyema kukamilisha zoezi hilo.

Kwa upande wake Mwakulonda amewashukuru wanachama wa Odm Msambweni kwa kumchagua ili kukiwakilisha chama Agosti.

Maeneo mengine yalitekeleza mchujo huo katika nyadhfa ya uwakilishi wadi ni Tiwi ambapo atakae wakilisha Odm katika uchaguzi ujao ni Ali Mwatando,Wadi ya Gombato Bongwe akiwa Hassan Mwasipho, wadi ya Kinondo akiwa Mambo Abdalla na Ukunda akiwa Omar Kitengele.